LIBYA-SIASA-USALAMA

Libya: Serikali ya Tobruk yajiuzulu baada ya maandamano dhidi ya uhaba wa bidhaa mahitajio

Maandamano ya watu wenye hasira huko Benghazi, Libya, Septemba 12, 2020.
Maandamano ya watu wenye hasira huko Benghazi, Libya, Septemba 12, 2020. Abdullah DOMA / AFP

Baada ya siku nne za maandamano ya watu wenye hasira kutokana na uhaba wa bidhaa mahitajio na kuzorota kwa huduma za umma, serikali ya Tobruk imeamua kujiuzulu, baada ya kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa bunge la nchi hiyo Jumapili Septemba 13.

Matangazo ya kibiashara

Taasisi hizi zinatawala sehemu ya Libya inayodhibitiwa na Marshal Khalifa Haftar lakini hazitambuliwi na jamii ya kimataifa.

Hatua ya kujiuzulu kwa serikali ya mpito inayoongozwa na Abdallah al-Thani ilitangazwa kufuatia mwito wa dharura uliyotolewa kwa serikali na Aguila Saleh , spika wa Bunge lenye makao yake huko Tobruk.

Aguila Saleh anaendelea na mazungumzo makubwa ya kuunda serikali moja na ya kweli ya umoja wa kitaifa, ili kurekebisha Baraza la rais na kutoa sawa nyadhifa kwenye uongozi wa taasisi huru za Libya kati ya majimbo mitatu inayounda Libya.

Msemaji wa Bunge ametangaza kuwa uamuzi kuhusu serikali hii utachukuliwa katika kikao cha Bunge kitakachohusika na suala hili bila kutaja tarehe. kwa kusubiri, ataendelea kusimamia mambo ya dharura.

Kujiuzulu huko kunakuja baada ya maandamano ya siku nne mashariki mwa Libya dhidi ya hali duni ya maisha ya kiuchumi na kijamii. Maandamano haya yalianza huko Tripoli na magharibi mwa nchi mwezi uliopita.