DRC-USALAMA

Machafuko Kivu Kusini: Karibu makundi 70 yenye silaha yakutana Bukavu

Mji mkuuwa mkoa wa Kivu Kusini, wa Bukavu, DRC.
Mji mkuuwa mkoa wa Kivu Kusini, wa Bukavu, DRC. Wikimedia/EMMANRMS

Wawakilishi wa makundi 70 yenye silaha wanakutana tangu Jumatatu huko Murhesa katika eneo la Kabare, karibu na mji wa Bukavu, katika Mkoa wa Kivu Kusini, kujadili maswala ya usalama na mchakato wa kuwapokonya silaha wapiganaji (DDR).

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo umeandaliwa na mashirika matatu yasio ya kiserikali yaliyobobea katika utatuzi wa migogoro.

Hii ni mara ya kwanza mkutano wa aina hii kufanyika kwa kiwango kama hicho cha uwakilishi kutoka upande wa serikali.

Katika siku ya kwanza ya mkutano huo, walishiriki mkutano huo, Waziri wa Ulinzi, afisa wa idara ya ujasusi katika ngazi ya taifa, Waziri wa Mambo ya Ndani katika mkoa wa Kivu Kusini na karibu wawakilishi wa makundi yote yenye silaha na wajumbe kutoka jamii zilizo kwenye mizozo zimliwakilishwa.

Mkutano wa kwanza ulifanyika katika parokia ya Murhesa mwezi Desemba wakati serikali ilikuwa iliwakilishwa kwa kiwango cha chini. Mapendekezo kadhaa yalitolewa katika mkutano huo na orodha ya hatua kadhaa zilichukuliwa lakini hazikutekelezwa.

Kiongozi wa shirika la Search For Common Ground huko Bukavu, Koffi Gervais, ana imani kwamba mkutano hiuo utazaa matunda. "Tumegundua kuwa ahadi zote tunazotoa katika suala la maendeleo, ikiwa hatutazingatia suala la mshikamano wa kijamii na mabadiliko ya mizozo, hii ina hatari ya kusababisha athari kwa mienendo ya mshikamano wa jamii. Mwezi Desemba tulilazimika kufanya mkutano ambao tuliuita 'Murhesa 1' ambapo mapendekezo kadhaa yalitolewa,lakini kutokana na ugonjwa wa COVID-19, hatukuweza kufikia kutekeleza hatua tulizokubaliana. Hii ndio sababu timetoa wito tena kwa mamlaka katika ngazi ya juu, katika ngazi ya kitaifa, kwa ushiriki wao mzuri ".

Lakini kuongezeka kwa makundi yenye silaha kunachanganya hali ya usalama kuzorota zaidi. kutoka makundi 38 mwezi Desemba na kufikia leo makundi karibu 70, hasa kwa sababu ya mgawanyiko kutokana na malumbano ya ndani.