MALI-SIASA-USALAMA
Mali: Rais wa zamani Moussa Traoré aaga dunia
Imechapishwa:
Rais wa zamani wa Mali Moussa Traoré amefariki dunia Jumanne (Septemba 15), chanzo kutoka familia yake kimeiambia RFI.
Matangazo ya kibiashara
Moussa Traoré, ambaye alizaliwa Septemba 25, 1936, alichukua hatamu ya uongozi wa nchi mwaka 1968 kabla ya kupinduliwa mwezi Machi 1991.
Moussa Traoré alihukumiwa kifo, lakini mwaka 2020 rais wa zamani Alpha Oumar Konaré alimsamehe. Katika miaka ya hivi karibuni, amekuwa akisikilizwa sana miongoni mwa wanasiasa nchini Mali.
(Habari zaidi katika sasa zijazo)