ALGERIA-RSF-HAKI

Mwandishi wa habari wa Algeria Drareni ahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela

Mwandishi wa habari wa Algeria Khaled Drareni akibebwa kama kama mfalme, Machi 6, 2020 wakati wa maandamano ya kuipinga serikali.
Mwandishi wa habari wa Algeria Khaled Drareni akibebwa kama kama mfalme, Machi 6, 2020 wakati wa maandamano ya kuipinga serikali. RYAD KRAMDI / AFP

Mahakama ya Rufaa nchini Algeria imemhukumu mwandishi wa habari wa Algeria Khaled Drareni kifungo cha miaka miwili jela kwa kutaka kuhatarisha usalama wa taifa na kuleta uchochezi kwa kuhimiza kundi lisilo na silaha.

Matangazo ya kibiashara

Hukumu hii kubwa aliyopewa mwandishi wa shirika la wanahabari wa Wasio na Mipaka (RSF) nchini Algeria, inaendana na matakwa ya ya mamlaka ambayo inataka kusiwepo na mtu mwengine atakaye thubutu kuingia mitaani sawa na maandamano yaliyosababisha kujiuzulu kwa rais Abdelaziz Bouteflika mwaka Aprili 2019, kulingana na mashirika ya haki ya binadamu.

RSF imelaani uamuzi "wa kipuuzi na ulio kinyume na sheria" na kutangaza kwamba miji mikubwa kadhaa ya Ufaransa, ikiwa ni pamoja na ule wa Paris kuanzia leo Jumanne jioni, wanatarajia kuweka turubai kwenye viunga vya kumbi za miji yao ili kuonyesha uungwaji wao mkono kwa mwandishi huyo.

Khaled Drareni alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani mwezi uliopita. Mwanahabari huyo, ambaye kwa zaidi ya mwaka mmoja alitoa habari zinazohusiana na maandamano ya kila wiki ya vuguvugu la "Hirak" dhidi ya utawala ulioko madarakani, alikamatwa mwezi Machi mwaka huu.

Maandamano haya yalilazimika kusitishwa kwa sababu ya janga la Corona lakini wanaharakati wengine wametoa wito yarejeshwe wakati masharti yaliyowekwa kudhibiti ugonjwa huo hatari yataondolewa.

Waandamanaji wa vuguvugu la "Hirak" wanadai wajiuzulu vigogo walioko madarakani wakisaidiwa na jeshi na badala yake kurejelewa kwenye nyadhifa zao na kizazi kipya cha viongozi.