DRC-KABILA-SIASA

Rais mtaafu wa DRC Joseph Kabila ashiriki kikao cha bunge kama seneta

Rais mtaafu wa DRC, Joseph Kabila.
Rais mtaafu wa DRC, Joseph Kabila. ©John WESSELS/AFP

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Joseph Kabila amekwenda katika bunge la nchi hiyo kwa mara ya kwanza kama Seneta baada ya kuondoka madarakani mwaka 2019.

Matangazo ya kibiashara

Kabila mwenye umri wamiaka 49, aliwasili katika bunge hilo akiwa amevalia vazi maalum la kumtambulisha na alionekana mwenye tabasamu na kupiga picha na maseneta wenzake.

Katiba ya DRC inaeleza kuwa rais mstaafu anakuwa Seneta wa maisha.

Rais huyo za zamani amehudhuria vikao hivyo, wakati huu kukiwa na mvutano kati ya muungano wake wa kisiasa wa FCC na CACH wa rais Felix Tshisekedi.