COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Uchaguzi wa urais Côte d'Ivoire: Ouattara aidhinishwa kuwania kiti cha urais, Gbagbo akataliwa

Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara.
Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara. John MacDougall/Pool via REUTERS/File Photo

Nchini Côte d'Ivoire, Mahakama ya Katiba imemuidhinisha rais anayemaliza muda wake Alassane Ouattara kuwania kwenye kiti cha urais katika uchaguzi wa urais kwa muhula mwingine. Guillaume Soro na Laurent Gbagbo, hawakuidhinishwa.

Matangazo ya kibiashara

Faili arobaini na nne zilikuwa zimewasilishwa kwa Mahakama ya Katiba, lakini imepitisha nne ndizo zimepokelewa, ikiwa ni pamoja na ile ya rais Ouattara.

Mgombea urais wa chama cha PDCI, Henry Konan Bédié, pia ameidhinishwa, sawa na mgombea wa chama cha SPI, Pascal Affi N'Guessan, na Kouadio Konan Bertin, anayejulikana zaidi kwa herufi za mwanzo za majina yake KKB, aliyejitenga na chama cha PDCI.

Siku ya Jumapili kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro aliteuliwa kupeperusha bendera ya chama chake katika uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba.

Soro, ambaye yuko uhamishoni nchini Ufaransa, aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu aliteuliwa na chama chake cha Generations and People in Solidarity siku ya Jumapili.