COTE D'IVOIRE-SORO-HAKI

Cote d'Ivoire: Mahakama ya Afrika yaomba Guillaume Soro aweze kuwa mgombea

Mahakama hiyo iliiamuru Cote d'Ivoire isimamishe hati yake ya kukamatwa kwa Guillaume Soro na kuwaachilia ndugu zake 19 ambao walikuwa wamefungwa kwa miezi kadhaa.
Mahakama hiyo iliiamuru Cote d'Ivoire isimamishe hati yake ya kukamatwa kwa Guillaume Soro na kuwaachilia ndugu zake 19 ambao walikuwa wamefungwa kwa miezi kadhaa. ISSOUF SANOGO / AFP

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) imeitaka Côte d'Ivoire kumruhusu kiongozi wa zamani wa waasi na Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Guillaume Soro kugombea kwenye kiti cha urais katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 31.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu Mahakama ya Kati ilichukuwa uamuzi wa kutomuweka Guillaume Soro kwenye orodha ya wagombea katika uchaguzi wa urais nchini Côte d'Ivoire, ikibaini kwamba hatimizi vigezo vya kuwania katika uchaguzi huo.

Mwezi Aprili 200 Cote d'Ivoire ilitangaza kujiondoa katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, ikidai kwamba Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu imedhoofisha uhuru wake.

Wakati huo mahakama hiyo iliiamuru Cote d'Ivoire isimamishe hati yake ya kukamatwa kwa Guillaume Soro na kuwaachilia ndugu zake 19 ambao walikuwa wamefungwa kwa miezi kadhaa.

Mahakama nchini Cote d'Ivoire Soro ilimhukumu Guillaume Soro kifungo cha miaka 20 gerezani.

Soro, 47, ambaye pia ni waziri mkuu wa zamani, alipatikana na hatia ya kuficha na kutapeli fedha za umma.

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ni mahakama ya kimataifa iliyoanzishwa na nchi za Afrika ili kuhakikisha ulinzi wa haki za binadamu na watu barani Afrika.

Itifaki ya Uanzishwaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ilipitishwa Ouagadougou, Burkina Faso, mnamo Juni 9, 1998 na ilianza kutumika mnamo Januari 25, 2004.