AFRIKA KUSINI-CORONA-UFISADI-UCHUMI

Makanisa ya Afrika Kusini yalaani ufisadi uliokithiri

Padri wa Kanisa Katoliki nchini Afrika Kusini Aprili 9, 2020 huko Mabopane.
Padri wa Kanisa Katoliki nchini Afrika Kusini Aprili 9, 2020 huko Mabopane. AFP Photos/Phill Magakoe

Nchini Afrika Kusini, wengi wanajiuliza kuhusu usimamizi wa fedha zilizotolewa kwa mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa COVID-19, na ufisadi uliokithiri.

Matangazo ya kibiashara

Baraza la Makanisa nchini Afrika Kusini (SACC) limlaani vitendo hivyo vya ufisadi na kusema kuwa hakuna aliye juu ya sheria.

Maaskofu, wachungaji, na wawakilishi wengine wa makanisa tofauti ya Kikristo walifanya maandamano, Jumanne wiki hii wakiwa wamebebelea mabango walioandika maneneo yanayolaani vitendo vya ufisadi vinavyoendelea nchini Afrika Kusini.

Viongozi hao walisalia kimya kwa dakika kadhaa kuonyesha hasira waliyonayo kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo ambavyo, 'vinawaumiza raia wa chini'.

Maanfdamano hayo yalishuhudiwa katika miji mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Cape Town na Pretori.

Viongozi wa dini tayari waliandamana katika wiki za hivi karibuni wakilaani vitendo vya rushwa aua ufisadi vinavyoendelea serikalini, na athari kwa maisha ya walio hatarini zaidi wakati huu nchi hiyo ikikabiliwa na ugonjwa wa Covid-19.

Hayo yanajiri wakati utafiti wa watalaam wa afya nchini Afrika Kusini, umebaini kuwa watu Milioni 12 waliambukizwa virusi vya Corona, katika taifa hilo ambalo limeongoza kwa maambukizi zaidi barani Afrika.