MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Mali: ECOWAS yataka uteuzi wa rais na waziri mkuu kabla ya kuondolewa vikwazo

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, wa rais wa sasa wa ECOWAS, Septemba 15, 2020 huko Accra.
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, wa rais wa sasa wa ECOWAS, Septemba 15, 2020 huko Accra. REUTERS/Francis Kokoroko

Jumuiya ya Kiuchumi a Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, imewataka wanajeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali kufanya uteuzi wa haraka wa rais wa mpito wa nchi hiyo na waziri wake mkuu.

Matangazo ya kibiashara

ECOWAS inataka rais wa mpito na waziri mkuu wawe ni raia na hapana wanajeshi, kama kundi hilo la wanajeshi linavyopendekeza.

ECOWAS imebaini kwamba inataka uteuzi huo ufanyike haraka kabla ya kuondolewa kwa vikwazi vilivyowekewa nchi hiyo, siku chache tu baada ya mapinduzi yaliyoangusha utawala wa Ibrahim Boubacar Keita.

Huo ni msimamo wa ECOWAS wakati wa mkutano wake mdogo wa dharura kuhusu Mali uliofanyika Jumanne Septemba 15 katika mji mkuu wa Ghana , Accra, mkutano ambao ulihudhuriwa na marais 9 kutoka nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Kulingana na duru za kuaminika mpatanishi kutoka ECOWAS, Goodluck Jonhatan, rais wa zamani wa Nigeria, anatarajia kuzuru tena nchini ya Mali wiki ijayo.