MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Mali: Jeshi launga mkono kipindi cha mpito kuongozwa na mwanajeshi

Kanali-Meja Ismael Wagué, msemaji wa CNSP kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Bamako, Septemba 16, 2020.
Kanali-Meja Ismael Wagué, msemaji wa CNSP kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Bamako, Septemba 16, 2020. MICHELE CATTANI / AFP

Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano wiki hii, viongozi wa kijeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali, kwa mara ya kwanza, wamebaini rasmi kwamba nanaunga mkono kipindi cha mpito kitakachoongozwa na mwanajeshi.

Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mkutano, viongozi hao wa kijeshi pia walirejelea kuhusu yaliyozungumzwa katika mkutano wao wa mwisho huko Accra.

Hii ni mara ya kwanza kundi la wanajeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali tangu Agosti 18, kusema rasmi.

Wanajeshi hao wanaungana na maoni ya baadhi ya raia nchini humo ambao wanataka kipindi cha mpito kiongozwe na mwanajeshi. Lakini sasa wanalazimika kuzingatia ombi la Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, ambayo inataka uteuzi wa raia kama rais na waziri mkuu, ameripoti mwandishi wetu huko Bamako, Serge Daniel.

"Hoja zote ziko mezani," amesema Kanali-Meja Ismaël Wagué, msemaji wa kundi la wanajeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali. Msimamo wa ECOWAS ni miongoni mwa mada zinazojadiliwa. Kuna mambo ambayo yanatakiwa kufanywa, kuna jitihada ambazo zinatakiwa kufanywa. "

Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi waliwataka viongozi wa kijeshi nchini Mali, kukabidhi madaraka haraka kwa raia, baada ya mazugumzo yaliyofanyika siku ya Jumanne jijini Accra nchini Ghana.

Wakuu wa nchi za ECOWAS, walikuwa wametaka rais wa kiraia kupatikana kufikia Jumanne wiki hii, lakini hilo limegonga mwamba.

Mwenyekiti wa ECOWAS Nana Akufo-Addo, ambaye pia ni rais wa Ghana, alisema hakuna mwafaka wowote uliopatikana na ujumbe wa wasuluhishi utakwenda jijini Bamako wiki ijayo kwa mazungumzo zaidi, huku wakiwa na matumaini kuwa suluhu itapatikana.

Viongozi wa kijeshi nchini Mali walimwondoa madarakani rais Ibrahim Boubacar Keita, na wamekuwa wakipata shinikizo za kurejesha madaraka kwa raia.