KENYA-SIASA-UCHUMI

Kenya: Huduma za umma zazorota Kenya baada ya ufadhili wa kaunti kuzuia

Mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Mei 17, 2017.
Mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Mei 17, 2017. Photo by Thomas Imo/Photothek via Getty Images

Kenya imeingia katika mgogoro wa kisiasa ambao unatishia kugeuka haraka kuwa mgogoro wa kijamii. Kulingana na Katiba ya mwaka 2010, nchi hiyo imegawanyika katika kaunti 47 ambazo zinapaswa kupokea 15% ya mapato ya serikali.

Matangazo ya kibiashara

M

"Fedha zetu ziko wapi? " Seneta Aaron Cheruiyot aliuliza Alhamisi wiki hii. Kwa wiki kadhaa, mijadala inaendelea katika Bunge la Seneti nchini Kenya.Maseneta wanashughulikia mradi mpya wa usambazaji wa bajeti kati ya kaunti 47. Nakala hii inaeleza kugawana fedha kulingana na idadi ya watu. Baadhi ya maseneta wanapinga, wakiwa na hofu kwamba maeneo yenye watu wachache, mara nyingi masikini zaidi, yataumia.

Kutokana na hali, Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana, Wycliffe Oparanya, ametangaza kusimamishwa kwa sehemu ya huduma za umma. Almelezea kuwa baadhi ya maafisa hawakuwa na mishahara tena, na hakuna bima tena. Vituo vya afya vimeishiwa na dawa. Deni la dola milioni 18 limewasuilishwa na kampuni ya kuuza umeme. Kama matokeo, huduma ambazo sio muhimu zimesimamishwa.

Baraza linapendekeza wafanyakazi wasimamishekazi kwa wiki mbili. Shuguli zinatarajia kukwama katika hospitali mbalimbali, katika sekta ya ujenzi wa barabara au ukusanyaji wa taka. Uamuzi wa kutatanisha unaopingwa na baadhi maseneta kama Moses Wetangula, kiongozi wa chama cha FORD, ambaye anamtuhumu Wycliffe Oparanya kwa matumizi mabaya ya madaraka. Bodi ya Magavana sio mwajiri wa wafanyakazi wa umma. "Haiwezi hata kumuomba mfagiaji aache kufanya kazi," amesema.

Wengine wamechukua msimamo usioegemea upande wowote, kama Seneta Alfred Mutua, ambaye amelaani mgogoro wa kusikitisha. "Miaka 60 baada ya uhuru, hatuwezi hata kutatua matatizo yetu ya kisiasa na kiuchumi," amesema.

Siku ya Jumanne, rais Kenyatta alitoa nyongeza ya dola milioni 460 kwa kaunti zilizoadhibiwa. Lakini maseneta bado hawajaweza kufikia makubaliano. Wakati huo huo, nchi imetumbukiwa katika mgogoro.

iezi mitatu baada ya kuanza kwa mwaka mpya wa fedha, pesa hizo bado hazijatolewa. Kama matokeo, Bodi ya Magavana, chombo kinachowakilisha kaunti, kimetangaza kusimamishwa kwa sehemu ya huduma za umma.