DRC-USALAMA

Milio mingi ya risasi yasikika katika eneo la Fizi, Mashariki mwa DRC

Maeneo ya Fizi ena Baraka (Kivu Kusini).
Maeneo ya Fizi ena Baraka (Kivu Kusini). Google Maps

Mapigano yameripotiwa usiku wa Alhamisi kuamkia leo Ijumaakatika eneo la Fizi katika mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yanatokea saa chache baada ya makundi ya waasi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutia saini wiki hii kwenye mkataba wa kusitisha mapigano.

Mkataba huo unaeleza uundwaji wa kamati za ufuatiliaji zitakazohusika na kutathmini uheshimishwaji wa mkataba wa usitishwaji wa mapigano na kutengeneza ramani za maeneo yenye ukosefu wa usalama kwa kutambua wahusika na kuwafikisha mbele ya vyombo husika.

Haijajulmikana hasara ya mapigano hayo lakini, mashahidi wanasema kuwa walisikia milio mingi ya risasi na zana nzito nzito za kijeshi katika eneo hilo la Fizi.

Mkoa wa Kivu Kusini umeendelea kukumbwa na mashambulizi ya makundi yenye silaha, huku raia ndio wakiendelea kupoteza katika mashambulizi hayo.