SOMALIA-SIASA-USALAMA

Somalia yampata waziri mkuu mpya

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, kwa jina maarufu Farmajo, hapa ilikuwa huko New York , Septemba 23, 2019.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, kwa jina maarufu Farmajo, hapa ilikuwa huko New York , Septemba 23, 2019. Riccardo Savi / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, amemteua Mohamed Hussein Roble kuwa Waziri Mkuu, kuelekea Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwaka ujao.

Matangazo ya kibiashara

Roble sio mwanasiasa, ni Mhandisi ambaye amekuwa akifanya kazi katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi ILO.

Anachukua nafasi ya Hassan Ali Khaire, aliyefutwa kazi mwezi Julai baada ya kutofautiana na rais Farmajo kuhusu maandalizi ya Uchaguzi huo.

Hivi karibuni Umoja wa Ulaya, EU, ulisema kuwa unaghadhabiswa na hatua ya kumfuta kazi Waziri Mkuu wa Somalia Hassan Ali Khaire, ukibaini kwamba kuachishwa kazi kwa Waziri Mkuu ni utaratibu ulio kinyume na katiba.

Rais Mohamed Abdullahi Mohamed anaongoza taifa ambalo limeendelea kukabiliwa na chanagmoto za kiusalama kutokana na kuwepo kwa kundi la Al Shabab lakini pia mgogoro kati ya serikali ya Mogadishu na zile za majimbo.