GHANA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vya maambukizi vyapungua Ghana, baadhi ya shughuli za kawaida zarejelewa

Ghana imeendelea kushuhudia visa vya maambukizi vikipungua.
Ghana imeendelea kushuhudia visa vya maambukizi vikipungua. REUTERS/Francis Kokoroko

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo ametangaza kurejelewa tena kwa shughuli zote za michezo nchini humo baada ya nchi hiyo kuanza kushuhudia kushuka kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, rais Addo amesema mipaka ya nchi hiyo itaendelea kufungwa pamoja na maeneo ya burudani kama baa na kumbi za kuangalia filamu.

Pamoja na kupungua kwa maambukizi nchini humo, rais huyo amewataka wananchi kuendelea kuvaa barakoa kila wakati.

Ghana ina maambukizi zaidi ya Elfu 46 na vifo 297 vilivyotokana na virusi vya Corona.

Virusi vya Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyojulikana kusababisha magonjwa yanayoanzia homa ya kawaida hadi homa kali kama vile Homa Kali ya Upumuaji ya Mashariki ya Kati (MERS) na Homa Kali ya Mfumo wa Upumuaji (SARS).

Virusi vipya vya Corona (COVID-19) viligunduliwa 2019 huko Wuhan, China. Hivi ni virusi vipya vya Corona ambavyo havijatambuliwa hapo awali kwa wanadamu.