MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Mali: Jeshi lakimbizana na muda kabla ya muda wa mwisho wa ECOWAS kufikia tamati

Assimi Goita, rais wa Baraza la Kitaifa la Wokovu la Watunchini Mali (CNSP), wakati wa mkutano wa ECOWAS huko Accra, Septemba 15, 2020.
Assimi Goita, rais wa Baraza la Kitaifa la Wokovu la Watunchini Mali (CNSP), wakati wa mkutano wa ECOWAS huko Accra, Septemba 15, 2020. Nipah Dennis / AFP

Wengi wanahiji iwapo Mali itakuwa imempata rais na waziri mkuu wa mpito hadi Jumanne asubuhi, muda wa mwisho uliyowekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, kabla vikwazo kuchukuliwa.

Matangazo ya kibiashara

ECOWAS iliwataka viongozi wa kijeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali tangu Agosti 18 kufanya uteuzi haraka wa rais na waziri mkuu wa mpito, ambao wote ni raia hadi Jumanne Septemba 22.

Wanajeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali wameendelea kukutana kwa mazungumzo na wadau wote katika mchakato wa amani nchini Mali.

Majadiliano haya yanatarajiwa kuhitimishwa na mkutano leo Jumatatu wa viongozi ambaohusika na kuteua viongozi wapya wa nchi ambo ni raia.

Lakini ni vigumu kusema kwa sasa ikiwa mkutano huu umeanza. Kwanza, kwa sababu mikutano yote inafayika kwa faragha na baadhi ya mikutano inanyika kwa wakati mmoja, baadhi ya mikutano hiyo inafanyika kwenye makao makuu ya Wizara ya Ulinzi, na mingine kwenye kambi ya jeshi ya Kati.

Kulingana na duru zetu, mikutano hii inalenga kupata makubaliano kuhusu jina kabla ya kuliwasilisha rasmi kwa wajumbe katika mikutano mbalimbali, labda kwa kuokoa muda, kwani imesalia tu ni saa chache tu kabla ya muda wa mwisho, Jumanne wiki hii. Takwimu kadhaa huzunguka juu ya idadi ya washiriki katika chuo hiki, zaidi ya kumi kwa hali yoyote.

Katika mikutano hiyo inayofanyika kwa wakati mmoja katika maeneo tofauti, Kamati ya Kitaifa ya Wokovu wa Watu (CNSP), inawakilishwa na wajumbe watano, vuguvugu la M5 linawakilishwa na watu wawili, mashirika ya kiraia yanawakilishwa na wajumbe wawili na wajumbe wawili kwa dini.

Kwa upande wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ambayo inaendelea kuweka shinikizo kwa wanajeshi wanaoshikilia madaraka raia aweze kuteuliwa hadi Jumanne hii kwenye nafasi ya rais. Goodluck Jonathan, mpatanishi wa ECOWAS, anasubiriwa Jumatano kutangaza hali inayojiri nchini Mali.

Wakati huo huo, Jumatatu hii jioni, Assimi Goïta, kiongozi wa wanajeshi wanaoshikilia madaraka, anatarajia kuhutubia taifa, hotuba ambayo itarushwa kwenye redio na runinga katika mkesha wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 60 ya uhuru wa Mali.