SUDAN-MAREKANI-USHIRIKIANO

Sudan: Mike Pompeo ataka Sudan iondolewe haraka vikwazo vya Marekani

Waziri wa Mambo ya Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo huko Washington, Aprili 29, 2020.
Waziri wa Mambo ya Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo huko Washington, Aprili 29, 2020. Andrew Harnik/Pool via REUTERS

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inaendelea na shinikizo la kutaka Sudan iondolewe katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi, ambazo ziliwekewa vikwazo na Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, ameomba maseneta wa Marekani kuiondoa Khartoum kwenye orodha ya nchi ambazo Marekani inaona kuwa zinafadhili ugaidi duniani, hatua ambayo ingerahisisha kuimarika kwa hali ya uchumi wa nchi hiyo ambao umedorora.

Mike Pompeo ameomba maseneta "kutumia fursa hii," kulingana na barua aliyoandika na kuchapishwa na Gazeti la The Foreign Policy.

Akizungumza na Mitch McConnell, kiongozi wa wengi kutoka chama cha Republican katika Bunge la Seneti la Marekani Jumatano wiki iliyopita, Mike Pompeo alibaini kwamba hii ni "fursa ya kipekee kuunga mkono kipindi cha mpito kinachoongozwa na raia nchini Sudan."

Aliomba maseneta kupitisha nakala iliyoandikwa na mjumbe wa chama cha Democratic ,Chris Coons, ifikapo katikati ya mwezi Oktoba. Uchumi wa Sudan unaendelea kudorora tangu Marekani kuchukuwa vikwazo mwaka 1993.

VIkwazo hivyo vinaizua Sudan kupata sehemu ya mfumo wa kifedha wa kimataifa. Mike Pompeo amekumbusha kwamba ni kwa masilahi ya Marekani na usalama wake kuzuia taasisi za mpito kushindwa kuwajibika, hali ambayo inaweza kusababisha kurudi kwa utawala wa Kiisilamu.

Nakala ya Seneta Coons inabaini kwamba Marekani inatakiwa kuiondoa Sudan kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi, na hivyo Marekani kupokea kutoka Sudan fidia ya dola milioni 335, hasa kwa familia za waathiriwa wa mashambulio ya 1998, dhidi ya balozi za Maekani nchini Kenya na Tanzania.