COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Uchaguzi wa urais Cote d'Ivoire: Upinzani waendelea na shinikizo dhidi ya Alassane Ouattara

Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire, Henri Konan Bédié Septemba 20, 2020 huko Abidjan.
Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire, Henri Konan Bédié Septemba 20, 2020 huko Abidjan. AFP/Issouf Sanogo

Wagombea wa upinzani wanaoawania urais nchini Cote d'Ivoire wameitisha mgomo na maandamano ya wananchi, kumshinikiza rais Alassane Ouattara kutowania urais kwa muhula wa tatu tarehe 31 mwezi Oktoba.

Matangazo ya kibiashara

Wakiongozwa na rais wa zamani Henri Konan Bedie, ambye anataka kurejea madarakani, baada ya kikao cha wagombea wa upinzani, mgombea huyo mkuu wa upinzani, amesema wameungana ili kumzuia rais Outtara kuwania tena urais kwa kile wanachosema ni kinyume cha Katiba ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Maandamano ya wapinzani dhidi ya rais Outtara ambaye aliidhinishwa na Mahakama kuwania tena wadhifa huo, yamekuwa yakiendelea katika siku zilizopita na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 10.

Rais Outtara ambaye alitarajiwa kutowania tena baada ya kumalizika mihula yake miwili, aliamua kuwania tena baada ya kifo cha ghafla cha Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly aliyekuwa ameteuliwa na chama tawala kumrithi.

Uchaguzi huo wa mwezi ujao, unaonekana kama kiipimo cha ukomavu wa kisiasa katika taifa hilo ambalo lilishuhudia machafuko ya baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu Elfu tatu.