LIBYA-UTURUKI-EU-USALAMA-SIASA

Ankara yashutumu vikwazo vya EU dhidi ya kampuni ya Uturuki kuhusu suala la Libya

Askari wa vikosi vya Khalifa Haftar akielekezea bunduki yake kwenye picha ya rais wa Uturuki Tayyip Erdogan iliyetundikwa kwenye gari la jeshi la Uturuki.
Askari wa vikosi vya Khalifa Haftar akielekezea bunduki yake kwenye picha ya rais wa Uturuki Tayyip Erdogan iliyetundikwa kwenye gari la jeshi la Uturuki. REUTERS/Esam Omran Al-Fetori

Uturuki imesema "kusikitisha sana" na uamuzi wa Umoja wa Ulaya wa kuiwekea vikwazo kampuni ya Uturuki kwa kukiuka vikwazo kuhusu uuzaji wa silaha ambavyo Umoja wa Mataifa uliweka dhidi ya Libya.

Matangazo ya kibiashara

Mpango wa ulinzi wa majini wa Umoja wa Ulaya, ambao unafanya shughuli zake katika pwani ya Libya, ndio uliokuja na matokeo ya tuhuma za makampuni hayo, baada ya kukusanya taarifa za kijasusi za ukiukwaji wa sheria za kimataifa.

"Wakati ambapo juhudi zinafanywa kupunguza uhasama katika Mediterania ya Mashariki, kuchukua uamuzi huo mbaya ni jambo la kusikitisha sana," Wizara ya Mambo ya nje ya Uturuki imesema katika taarifa, ikibaini kwamba uamuzi huo "haukuwa na thamani yoyote" kwa Ankara.Umoja wa Ulaya imeweka vikwazo dhidi ya makampuni matatu (moja ya Uturuki, moja ya Jordan na nyingine moja ya Kazakh) na mbili za Libya zilizohusishwa na suala la Libya, vyanzo vya kidiplomasia vimeliambia shirika la habari la AFP mapema huko Brussels.

Katika mkutano wao wa Brussel, mawaziri wa mambo ya nje wa umoja huo wametia saini hatua ya kuzizuia mali zozote za Umoja wa Ulaya ambazo zipo katika himaya ya makampuni hayo, kuzuia masoko ya kibiashara na kupiga marufuku kabisa kufanya biashara yoyote na mataifa wanachama wa umoja huo.

Mawili miongoni mwa makampuni hayo pia yamewekewa vikwazo kutokana na ukiukaji wa haki za binaadamu nchini Libya, katika kipindi ambacho serikali inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa ilipovamiwa na mbabe wa kivita wa masahiriki mwa Libya, Khalifa Haftar.