DRC-ITURI-USALAMA

Ituri: Wanamgambo 13 wauawa katika mapigano kati ya jeshi la FARDC na FPIC

Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006.
Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006. REUTERS

Wanamgambo 13 kutoka kundi lenye silaha la FPIC wameangamizwa na wanajeshi wa serikali, FARDC, huko Babode na Beabo katika eneo la Babelebe katika wilaya ya Irumu.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo kutoka eneo hilo, mapigano kati ya pande hizo mbili siku ya Jumanne (Septemba 22) yalidumu karibu saa nne.

Mashambulizi yalizinduliwa tangu Jumatatu, Septemba 21 na vikosi vya serikali dhidi ya washambuliaji hao katika ngome yao moja iliyoko katika eneo la Ngongo.

Kulingana na Redio Okapi (redio ya Umoja wa Mataifa nchini DRC) ikinukuu mkazi mmoja iliomhoji kwa njia ya simu, watu kadhaa walikimnia katika maeneo ya Mwanga na Tuma. Vyanzo vingine vimebaini kwamba watu 13 wameangamaia katika mapigano hayo na silaha tano zilikamatwa na vikosi vya serikali.

Hadi leo Jumatano asubuhi, watu wengine wamekuwa hawajarudi makwao kwa kuhofia kwamba huenda wapiganaji hao wakaja kulipiza kisasi.

Msemaji wa jeshi katika mkoa wa Ituri, Luteni Jules Ngongo, amebaini kwamba operesheni hiyo ilikuwa ya kuwasaka wanamgambo wa kundi la FPIC ambao wanahatarisha usalama katika eneo hilo la wilaya ya Irumu. Amesema kuwa wanamgambo watano waliuawa, silaha aina ya AK47 na risasi kadhaa vilikamatwa.Kulingana na mashahidi, visa kadhaa vya uporaji wa mali ya raia pia viliripotiwa.