COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Rais Alassane Ouattara aendelea kukabiliwa na shinikizo la kutowania kiti cha urais

Affi N'Guessan, amemuwelezea rais Outtara kama dikteta anayetaka kuendelea kuwa madarakani.
Affi N'Guessan, amemuwelezea rais Outtara kama dikteta anayetaka kuendelea kuwa madarakani. SIA KAMBOU / AFP

Mgombea mwingine wa urais nchini Côte d’Ivoire ambaye pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu Pascal Affi N'Guessan, ameugana na mgombea mwingine wa upinzani Henri Konan Bedie, kuwataka wananchi wa taifa hilo kugoma na kuadamana ili kumshinikiza rais Alassane Ouattara kutowania urais kwa muhula wa tatu.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo umepangwa kufanyika mwezi Oktoba, na upinzani unasema hatua ya rais Ouattara kuwania tena na kuidhinishwa na Mahakama, ni kinyume cha Katiba ya nchi hiyo.

Affi N'Guessan, amemuwelezea rais Outtara kama dikteta anayetaka kuendelea kuwa madarakani.

Nacho chama cha Outtara kimesema uchaguzi utafanyika hata kama utasusiwa na upinzani.

Hivi karibuni Mahakama ya Katiba ilimuidhinisha rais anayemaliza muda wake Alassane Ouattara kuwania kwenye kiti cha urais katika uchaguzi wa urais kwa muhula mwingine.