DRC-UCHUMI-USHIRIKIANO

Rais wa DRC ataka mataifa masikini kusamehewa mzigo wa madeni

Rais wa DRC Félix Tshisekedi atoa wito kwa mataifa tajiri kusamehe madeni kwa mataifa masikini.
Rais wa DRC Félix Tshisekedi atoa wito kwa mataifa tajiri kusamehe madeni kwa mataifa masikini. Sumy Sadurni / AFP

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ameomba mataifa tajiri kutoa msamaha wa madeni kwa mataifa masikini yanayoendelea kupambana na janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Tshisekedi amesema hatua hiyi itasaidia mataifa hayo kama DRC, kuendeleza uchumi wake baada ya janga hili ambalo limeleta madhara makubwa ya kiuchumi katika mataifa masikini na yanayoendelea hasa barani Afrika,wakati nchi yake ikiwa na maambukizi zaidi ya Elfu 10 ya Corona.

Licha ya mataifa tajiri zaidi ya 20 na Shirika la Fedha Duniani, IMF, kusema kuwa yanathathmini cha kufanya kuyasaidia mataifa hayo, rais Thsisekedi katika ujumbe wake kwa viongozi wa dunia kupitia njia ya video, ametaka kufutwa kabisa kwa madeni hayo.

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo linadaiwa kuwa miongoni mwa mataifa masikini duniani licha ya utajiri wake wa rasimali na imekuwa ikitegemea misaada ya mikopo kutoka nchi jirani kuendesha uchumi wake.

Suala la ukosefu wa usalama, hasa Mashariki mwa nchi hiyo na uongozi mbaya katika miaka iliyopita, zinaelezwa kuwa chanzo kikubwa cha umasikini huo.