DRC-LUBUMBASHI-USALAMA

DRC: Mji wa Lubumbashi wakumbwa na mapigano

Katikati mwa mji wa Lubumbashi.
Katikati mwa mji wa Lubumbashi. Wikimedia Commons CC BY-SA 2.5 Oasisk

Kumetokea mapigano kati ya kundi la wanamgambo wa Maï-Maï na vikosi vya jeshi la serikali, FARDC, katikati mwa mji mkuu wa Katanga, ya zamani Kusini Mashariki mwa DRC.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yametokea usiku wa Ijumaa kuamkia leo Jumamosi. Milio ya risasi na milipuko imeendelea kusikika mapema leo Jumamosi aljafajiri karibu na Chuo Kikuu.

Wanamgambo hao waliingia katika mji wa Lubumbashi usiku wakipitia maeneo kadhaa ya mji huo. Vyanzo vya polisi, vilivyothibitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani katika mkoa huo, Philibert Kunda Milundu, vinahakikisha kuwa wapiganaji hao ni kutoka kundi la wanamgambo la Bakata Katanga, lililojitenga kutoka kundi la Maï-Maï.

Waziri Kunda Milundu amesema wanajeshi wamegizwa kutowapiga risasi wanamgambo hao. Hali ya wasiwasi pia inaripotiwa katika mji wa Likasi. Mapigano hayo yanatokea baada ya jaribio la wafungwa kutoroka kutibuliwa siku ya Ijumaa katika gereza la Kasapa huko Lubumbashi.