CAR-USALAMA-SIASA

CAR: Rais Touadera kuwania kiti cha urais kwa muhula wa pili

Rais Touadera,kupitia chama cha MCU, kimesema kuwa kiongozi huyo anaingia rasmi katika orodha ya wagombea wa uchaguzi huo uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Desemba.
Rais Touadera,kupitia chama cha MCU, kimesema kuwa kiongozi huyo anaingia rasmi katika orodha ya wagombea wa uchaguzi huo uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Desemba. REUTERS/Sergei Karpukhin

Rais wa Jamuhuri ya afrika ya Kati Faustin Archange Touadera, ametangaza nia yake ya kuwania tena uongozi wa nchi hiyo kwa muhula wa pili.

Matangazo ya kibiashara

Rais Touadera,kupitia chama cha MCU, kimesema kuwa kiongozi huyo anaingia rasmi katika orodha ya wagombea wa uchaguzi huo uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Desemba.

Rais wa zamani Francois Bozize naye pia amejitosa katika kinyanyang'anyiro hicho, katika nchi hiyo ambayo inaendelea kupigania utulivu na amani kwa miaka kadhaa sasa.

Hivi karibuni rais wa zamani wa mpito Catherine Samba-Panza, ambaye hana uhusiano wowote na chama chochote cha siasa, naye pia alitangaza kuwania kiti cha urais katika uchaguzi huo.

Catherine Samba-Panza aliteuliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi Januari 2014, ilipokuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Catherine Samba-Panza, ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika madaraka katika nchi hii ya Afrika ya Kati, alitoa nafasi kwa Faustin-Archange Touadéra, mshindi wa uchaguzi wa mwezi Machi 2016 na ambaye anapewa na fasi ya kuwania katika uchaguzi huo kwa muhula wa pili mwezi Desemba.