NIGERIA-MAUAJI-USALAMA

Watu 30 wauawa katika shambulio dhidi ya msafara wa Gavana wa Borno

Magaidi walishambulia msafara wa Gavana wa Borno , Babagana Umara Zulum karibu na mji wa Baga pembezoni lwa Ziwa Chad.
Magaidi walishambulia msafara wa Gavana wa Borno , Babagana Umara Zulum karibu na mji wa Baga pembezoni lwa Ziwa Chad. Daily Trust

Idadi ya watu waliopoteza maisha Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, baada ya msafara wa Gavana kuvamiwa, imeongezeka na kufikia 30.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti kutoka kwa maafisa wa usalama, zinasema kuwa miili zaidi ilipatikana katika jimbo la Borno ambalo lilishuhudia shambulizi hilo.

Miili iliyopatikana ni ya maafisa 12 wa polisi, wanajeshi watano, wapiganaji wanne wanaoungwa na serikali pamoja na raia tisa.

Mbali na mauaji hayo, watu wengine 13 walijeruhiwa katika shambulizi hilo ambalo maafisa wa usalama wanasema walifanikiwa kuwashinda magaidi waliovamia msafara huo.

Magaidi walishambulia msafara wa Gavana wa Borno, Babagana Umara Zulum karibu na mji wa Baga pembezoni lwa Ziwa Chad.

Kundi la Islamic State, linaloendeleza shughuli zake katika eneo la Afrika Magharibi, linashukiwa kutekeleza shambulizi hilo.

Watu zaidi ya Elfu 36, wameuawa na wengine zaidi ya Milioni Mbili wameyakimbia makwao kutokana na mashambulizi ya ugaidi Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, kwa kipindi cha miaka 10 sasa.