DRC-USALAMA

Msafara wa amani waendelea mashariki mwa DRC

Moja ya mitaa ya mji wa Kalemi, katika mkoa wa Tanganyika, DRC, Machi 25, 2016.
Moja ya mitaa ya mji wa Kalemi, katika mkoa wa Tanganyika, DRC, Machi 25, 2016. RFI/Sonia Rolley

Kwa wiki moja wabunge katika ngazi ya taifa na waziri wa ulinzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaendelea na msafara wa amani Mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Jana, ujumbe huo uliwasili katika mji wa Kalemie katikamkoa wa Tanganyika ambapo mapigano kati ya wanamgambo kutoka jamii ya walio wachache ya Mbirikimo na Waluba yamekuwa yakitokea mara kwa mara.

Msafara huo unafayika katika maeneo yanayoshambuliwa hasa na kundi la waasi wa Uganda wa ADF, hali ambayo imeendelea kuzua gumzo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Msafara huo wa amai utapita katika mikoa ya Kivu Kusini, Kivu Kaskazini, Ituri na Tanganyika. Wabunge hao wanane na Waziri wa Ulinzi wameendelea kuzuru maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa vikosi vya usalama vya serikali.

Ujumbe huo hutakuna na makundi yenye silaha, kulingana na vyanzo vya usalama.

Ujumbe huo utawezesha wabunge kuona ukweli wa hali ya mambo. “Kuna vifo vingi, jamii zinahitaji mazungumzo. Na jeshi linapaswa kudhibiti maeneo yote ya nchi. Kwa kweli kunahitajika njia thabiti kwa kuepuka kurudi tena kwa ukosefu wa usalama, ”amesema Juvenal Munubo, mkuu wa ujumbe wa wabunge.

Mwenzake Bernard Kayumba amebainisha kuwa mzozo huo unachochewa na "watu au wanasiasa wanataka kuwepo na makundi ya wanamgambo katika mikoa tofauti".