AFRIKA-CORONA-AFYA

Hali ya kawaida yaanza kurejea Afrika, baada ya maambukizi kupungua

Muuguzi katika kitengo kinachotibu virusi vya Corona huko Mekele, Ethiopia, Septemba 7, 2020.
Muuguzi katika kitengo kinachotibu virusi vya Corona huko Mekele, Ethiopia, Septemba 7, 2020. AFP Photos/Eduardo Soteras

Hali imeanza kurejea katika hali ya kawaida hatua kwa hatua katika baadhi ya mataifa barani Afrika licha ya hofu ya kutokuwa kama hapo awali kabla ya virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Wakati mataifa mengi yakitangaza kupunguza hatua zao za kujilinda na COVID-19 na raia wanapata ahueni kidogo, licha ya  wataalam kuonya dhidi ya kuruhusu mafanikio ya bara hilo yapite kwa kuridhika.

Bara la Afrika linaelezwa kuvumilia janga la virusi vya Corona kwa maana ya maambukizo na vifo, ingawa uchumi wake umeharibiwa vibaya.

Kulikuwa na sherehe nyingi huko The Black and White Lifestyle Pub huko Soweto mwishoni mwa juma lililopita ikiwa ni wikiendi ya kwanza tangu kuondolewa kwa makataa ya kujizuia na maambukizi ya virusi vya Corona.

Afrika Kusini ndio nchi iliyoathirika zaidi katika bara la Afrika.