COTE D'IVOIRE-GBAGBO-SIASA

Mke wa rais wa zamani wa Cote d'Ivoire avinyooshea kidole cha lawama vikosi vya Ufaransa

Simone, anayejulikana kwa jina maarufu kama 'mwanamke mkakamavu' alikua amehukumiwa miaka 20 jela kwa uvamizi wa mamlaka ya serikali dhidi ya jukumu lake katika ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 uliosababisha vifo vya watu elfu 3.
Simone, anayejulikana kwa jina maarufu kama 'mwanamke mkakamavu' alikua amehukumiwa miaka 20 jela kwa uvamizi wa mamlaka ya serikali dhidi ya jukumu lake katika ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 uliosababisha vifo vya watu elfu 3. ISSOUF SANOGO / AFP

Simone Gbagbo mke wa rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbabgo amelishtumu jeshi la Ufaransa kwa kushindwa kumlinda wakati alipotaka kubakwa, kipindi alipokamatwa mwaka 2011, madai aliyotoa kwa mara ya kwanza mwaka 2016.

Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano maalum na Runinga ya France 24, Simone ametaka pia Uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 31 mwezi huu kuahirishwa, baada ya rais Alassane Ouattara kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu, suala ambalo limezua mvutano mkali wa kisiasa nchini humo.

Mwaka 2018 rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara alitangaza msamaha kwa Simone Gbagbo, wakiwemo watu wengine 800 ambao walikuwa wamefungwa jela miaka 20 kutokana na mzozo wa kisiasa mwaka 2010.

Simone, anayejulikana kwa jina maarufu kama 'mwanamke mkakamavu' alikua amehukumiwa miaka 20 jela kwa uvamizi wa mamlaka ya serikali dhidi ya jukumu lake katika ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 uliosababisha vifo vya watu elfu 3.

Vita hivyo vilimalizika baada ya mumewe, Laurent Gbagbo kukamatwa na Umoja wa Mataifa na jeshi la Ufaransa kumuunga mkono rais wa hivi sasa Rais Alassane Ouattara.