MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Kipindi cha mpito Mali: Jeshi lakubali kuachia moja ya majukumu makubwa ya kiongozi wao

Kanali Assimi Goïta (katikati), kiongozi wa mapinduzi na makamu wa rais wa mpito, Septemba 22, 2020.
Kanali Assimi Goïta (katikati), kiongozi wa mapinduzi na makamu wa rais wa mpito, Septemba 22, 2020. MICHELE CATTANI / AFP

Nchini Mali, hati ambayo itaandaa kipindi cha mpito kwa miezi 18 ijayo imechapishwa tangu Alhamisi hii, Oktoba 1 katika Gazeti rasmi la serikali.

Matangazo ya kibiashara

Hati hiyo inazingatia mahitaji muhimu kutoka kwa Jumuiya ay Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, juu ya mamlaka ya makamu wa rais wa mpito, Kanali Assimi Goïta, kiongozi wa mapinduzi nchini Mali.

Tofauti na toleo la awali la hati ya kipindi cha mpito, moja iliyochapishwa katika gazeti rasmi la serikali Alhamisi wiki hii haionyeshi kuwa makamu wa rais anaweza kuchukua majukumu ya rais wa mpito ikiwa kutatokea dharura. kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Mali wamekubali kufuta moja ya majukumu makubwa ya kiongozi wake, Kanali Assimi Goïta, kiongozi namba 2 katika kipindi cha mpito.

Hii ni moja ya masharti makuu yaliyotolewa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, ili kuweza kuondoa vikwazo dhidi ya Mali.

Hata hivyo Ibara ya 7 ya hati hiyo, ambayo inafafanua mamlaka ya makamu wa rais anayehusika na masuala ya usalama na ulinzi, haionyeshi wazi kwamba makamu wa rais hawezi kuchukuwa majukumu ya rais. Muda kipindi cha mpito ni miezi 18, kulingana na nakala hiyo, ambayo imebaini kwamba rais na makamu wa rais hawatawania katika uchaguzi wa urais na uchaguzi wa wabunge baada ya kipindi cha mpito.

Taratibu za kuunda Baraza la Mpito la Kitaifa, chombo cha kutunga sheria, pia zinaelezwa kwenye Ibara ya 13. Baraza hilo litaundwa na wajumbe 121. kiongozi atakuwa askari au raia. Lakini ECOWAS pia iliomba kuvunjwa kwa kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi. Kwa suala hili, itabidi kusubiri. Hati hiyo inabainisha kuwa itabaki hadi kuundwa kwa taasisi zote za kipndi cha mpito.