DRC-RWANDA-USHIRIKIANO-USALAMA

DRC: Rais Tshisekedi ajaribu kutuliza hali ya mambo katika swala la Karega

Mnamo Agosti 24, 1998, kulingana na Umoja wa Mataifa, waasi wa RCD na washirika wao wa jeshi la Rwanda waliwaua zaidi ya raia elfu moja katika vijiji vya Kivu Kusini.
Mnamo Agosti 24, 1998, kulingana na Umoja wa Mataifa, waasi wa RCD na washirika wao wa jeshi la Rwanda waliwaua zaidi ya raia elfu moja katika vijiji vya Kivu Kusini. JOHN WESSELS / AFP

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Félix Tshisekedi, amewataka wananchi wa DRC kuwa na subira baada ya balozi wa Rwanda kupuuzia mbali mauaji ya raia wa DRC huko Kasika, katika mkoa wa Kivu Kusini, mwaka 1998.

Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Rwanda Vincent Karega alikanusha kuhusika kwa wanajeshi wa Rwanda na kupinga yaliyomo kwenye ripoti ya iliyoitwa Mapping kama ilivyochapishwa na Kamesheni kuu ya UN. Hakuna hoja ya kumfukuza mwanadiplomasia huyu, amesema rais Tshisekedi mbele ya waandishi wa habari wa DRC waishio Brussels, nchini Ubelgiji. Kauli ya rais imezua sintofahamu nchini DRC.

"Hakuna maana ya kuzusha uhasama," rais amesema. Félix Tshisekedi amebaini kwamba mchakato katika ngazi ya kidiplomasia umeanza kuishinikiza Kigali kumuonya Vincent Karega.

Kwa upande wa Seneta anayemuunga mkono rais Kabila, Francine Muyumba, ambaye amekuwa amekuwa ameghadhibishwa kwa miezi kadhaa dhidi ya maneno yanayotolewa na wanadiplomasia wa kigeni jijini Kinshasa, amesema "Hatuwezi kufidia heshima ya taifa kwa kukidhi masilahi ya washirika."

Francine Muyumba ambaye pia ni Pia, mwenyekiti wa Tume ya ushirikiano katika Baraza la Seneti la DRC, alibani kwamba Vincent Karega alifanya "kosa kubwa" ambalo "linapaswa kushutumiwa wazi na mamlaka ya DRC".