MOROCCO-MAREKANI-USALAMA

Morocco na Marekani wanasaini mkataba wa ushirikiano wa kijeshi

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper akiwa na Waziri wa Mambo ya nje wa Morocco Nasser Bourita huko Rabat, Oktoba 2, 2020.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper akiwa na Waziri wa Mambo ya nje wa Morocco Nasser Bourita huko Rabat, Oktoba 2, 2020. AP Photo/Mosa'ab Elshamy

Waziri wa Ulinzi wa Marekani alimaliza ziara yake huko Afrika Kaskazini siku ya Ijumaa. Mark Esper alikuwa nchini Morocco, baada ya kuzuru Tunisia na Algeria wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya siku tatu ililenga kuimarisha ushirikiano wa kijeshi, vita dhidi ya makundi ya kijihadi na usalama katika kanda hiyo.

Ushirikiano wetu uko imara na umedumu," Waziri wa Mambo ya nje wa Morocco Nasser Bourita amesema baada ya kukutana kwa mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Marekani.

Mark Esper pia amekutana na mkuu wa majeshi ya Morocco na waziri wa ulinzi wa Morocco.

Mkataba wa ushirikiano wa kijeshi

Kama ilivyokuwa nchini Tunisia Jumatano, Septemba 30, Mark Esper amesaini mkataba wa miaka 10 ya ushirikiano wa kijeshi huko Rabat na Naibu Waziri anayesimamia Utawala na Ulinzi wa Kitaifa, Abdellatif Loudiyi. amebaini kwamba Marekani na Morocco zinafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu katika nyanja ya usalama.

Mkataba huu wa miaka kumi unafungua njia ya ushirikiano katika nyanja ya kimkakati ya kijeshi, ununuzi wa silaha na vifaa, mafunzo ya jeshi, na pia ujasusi kati ya nchi hizo mbili, ameripoti mwandishi wetu huko Casablanca, Nina Kozlowski.

Mark Esper alisisitiza hasa juu ya maswala ya ugaidi, vitisho kutoka nchi kwenda nyingine au kudorora kwa usalama katika kanda hiyo. Washington sasa inataka kushirikiana na washirika wa kuaminika barani Afrika ili kutuliza hali ya mambo, hasa nchini Libya na katika kanda ya Sahel.