COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Joto la kisiasa lapanda kuelekea uchaguzi wa urais Cote d'Ivoire

Kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwisho wa mwezi huu nchini Côte d’Ivoire, mgombea urais wa upinzani Kouadio Konan Bertin amezindua kampeni zake jijini Abidjan.

Mgombea urais nchini Côte d’Ivoire Kouadio Konan Bertin huko Abidjan, Oktoba 4, 2020.
Mgombea urais nchini Côte d’Ivoire Kouadio Konan Bertin huko Abidjan, Oktoba 4, 2020. AFP Photos/Sia Kambou
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya wafuasi wake walikusanyika jana Jumapili wakicheza muziki kabla ya kumsikiliza mgombea huyo aliyewaeleza ni kwanini ameamua kuwania urais na matarajio yake.

Bertin aliyewania tena urais mwaka huu, atapambana na wagombea wengine watatu, wakiwemo rais Alassane Ouattara pamoja na Henri Konan Bédié na Pascal Affi N’Guessan.

Uchaguzi unapoelekea kukaribia wanasiasa wa upinzani nao wameendelea kushinikiza kujiondoa katika kinyang'ayiro hicho rais Outtara anayewania kwa muhula wa tatu.

Hivi karibuni mgombea mwingine wa urais nchini Côte d’Ivoire ambaye pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu Pascal Affi N'Guessan, aliugana na mgombea mwingine wa upinzani Henri Konan Bedie, kuwataka wananchi wa taifa hilo kugoma na kuadamana ili kumshinikiza rais Alassane Ouattara kutowania urais kwa muhula wa tatu.

Uchaguzi huo umepangwa kufanyika mwezi Oktoba, na upinzani unasema hatua ya rais Ouattara kuwania tena na kuidhinishwa na Mahakama, ni kinyume cha Katiba ya nchi hiyo.

Affi N'Guessan, alimuwelezea rais Outtara kama dikteta anayetaka kuendelea kuwa madarakani.

Chama cha Outtara kimeendelea kusema uchaguzi utafanyika hata kama utasusiwa na upinzani.

Hivi karibuni Mahakama ya Katiba ilimuidhinisha rais anayemaliza muda wake Alassane Ouattara kuwania kwenye kiti cha urais katika uchaguzi wa urais kwa muhula mwingine.