SUDAN-MKATABA-USALAMA-SIASA

Shughuli zazorota katika Kaskazini mwa Karthoum

Mkuu wa Baraza Kuu la Sudan Abdel Fattah al-Burhan na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir wakishikana mikono wakati wa kutiwa saini kwa mkataba wa amani huko Juba tarehe 3 Oktoba 2020.
Mkuu wa Baraza Kuu la Sudan Abdel Fattah al-Burhan na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir wakishikana mikono wakati wa kutiwa saini kwa mkataba wa amani huko Juba tarehe 3 Oktoba 2020. REUTERS/Jok Solomun

Nchini Sudan, waandamanji siku ya jumapili,walifunga barabara za kuingia katika eneo la bandari, kaskazini mwa jiji la Khartoum ,wakilalamika kuhusu mkataba wa makubaliano uliotiwa saini baina ya serikali na baaddhi ya makundi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yaliotiwa saini Jumamosi Oktoba 3 jijini juba Sudan kusini, yalitazamiwa kumaliza mzozo ambao umekuwepo katika maeneo ya Dafur Magharibi na kusini mwa Kordofan.

Pande zote mbili zilitarajiwa kusaini mkataba huo mjini Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, ambayo imetoa mchango mkubwa wa ushauri kwa makundi ya waasi kuweka silaha chini kwa minajili ya kurejesha amani baada ya mapigano ya zaidi ya miaka thelathini.

Kusainiwa kwa mkataba huo kunakuja wakati ambapo nchi ya Sudan ina serikali mpya na mojawapo ya malengo yake ni kumaliza uasi nchini humo.

Ingawaje makundi tisa ya waasi yalisaini mkataba huo wa amani, kuna makundi mawili ambayo kufikia sasa yamekataa kusaini mkataba huo. Kundi moja ni Sudan Liberation Movement, la waasi lenye makao yake katika jimbo la Darfur na ambalo linaongozwa na Abdelwahid Nour.

Kundi la pili la Sudan Peoples Liberation Movement-North, lenye makao yake katika jimbo la Korodofan-Kusini na linaongozwa na Abdelaziz Hilu.