UTURUKI-LIBYA-USALAMA

Uturuki yaahidi mshikamano kamili na serikali ya umoja wa kitaifa Libya

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoga, ametangaza kuunga mkono serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa nchini Libya GNA. Rais Recep amesema haya akiwa katika mkutano kule Istanbul.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. Adem ALTAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Erdogan, alikutana na kiongozi wa serikali ya Tripoli, Fayez Al Sarraj ,ambaye mwezi jana alitangaza mipango ya kuwaachia madaraka katika kipindicha wiki sita zijazo kama njia moja ya mktaba wa makubalinao ya kuleta amani.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya wizara ya ulinzi ya Marekani, Uturuki imepeleka kati ya wapiganaji 3,500 na 3,800 nchini Libya katika kipindi cha miezi mitatu ya mwaka huu.

Ripoti hiyo ni ya kwanza kutoa maelezo ya jinsi Uturuki inavyopeleka wapiganaji ambao wanajaribu kusaidia kubadilisha mkondo wa vita nchini Libya.

Vita vya Libya ni vita vya washirika. Nchi nyingi za kigeni zinahusika katika suala hili. Uturuki na Urusi ni washirika wawili kati ya pande mbili hasimu katika mzozo huo.

Nchi hizo mbili zinaunga mkono kambi mbili zinazokinzana nchini Libya. Moscow inaunga mkono mbabe wa kivita mashariki mwa Libya, Marshal Haftar, wakati Ankara ikiunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa yenye makao makuu jijini Tripoli, na kambi ya Magharibi mwa Libya kwa ujumla. Nchi zote mbili hizi zimetuma idadi kubwa ya silaha na maelfu ya wanajeshi nchini Libya. Wapiganaji wanaojulikana kwa jina la "Wagner" na vile vile mamluki kutoka Syria wanaounga mkono Urusi, mamluki kutoka Syria na mataifa mengine mengi kwa upande wa Uturuki wako nchini Libya kusaidia pande mbili hasimu katika vita hivyo.

Kwa hiyo, Urusi na Uturuki zinashindana nchini Libya kama vile nchini Syria. Kila nchi inatafuta kuongeza ushawishi wake, huku ikijaribu kutafuta maelewano, bila hata hivyo kufanikiwa.

Mwezi Juni, Mawaziri wa Mambo ya nje na Ulinzi wa Urusi walipana ziara nchini Uturuki, lakini ilifutwa katika dakika za mwisho wakati mazungumzo yalilenga kusitisha vita. Wakati huo Urusi ilibaini kile ilichokiita kutokea kwa "tofauti kubwa".