Morocco: Polisi yawashilia wanamgambo 4 wa IS
Imechapishwa:
Polisi nchini Morocco,wametangaza kuwatia kizimbani washukiwa wanne wanaohusishwa na kundi la jihadi ambao kwa mujibu wa ripoti walikuwa wanapanga msururu wa mashambukizi nchini humo.
Washukiwa wote wanne ni wenye asili ya Morocco na wako chini ya umri wa miaka 25.
Wakati huo huo Malioni ya wanafunzi wamerejea shuleni nchini Morocco baada ya miezi saba ya kufungwa kwa shule nchini humo kutokana na maambukizi ya janga la Corona.
Wakiwa wamevalia barakoa, wanafunzi hao wa shule za upili na za msingi walionekana wenye furaha kutokana na hatua hiyo ya serikali ya kuwafungulia shule tena wakati wakihitajika kufuata masharti ya wizara ya afya.