SUDAN-BASHIR-HAKI

 Kesi ya Omar Al Bashir yaanza kusikilizwa

Aliye kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir.
Aliye kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir. Reuters

Kesi inayomkabili  Omar Bashir, aliyekuwa rais wa Sudan, imeaanza kusikilizwa tena jijini Khartoum, kwa tuhuma za kuhusika katika mapinduzi ya serikali ya mwaka wa 1989, mapinduzi ambayo yalimweka katika uongozi wa taifa hilo kwa miaka 30.

Matangazo ya kibiashara

Bashir pamoja na watu wengine ,wakiwemo maafisa wa jeshi na raia wanakabiliwa na mashataka hayo ya mapinduzi, huku ombi lake la kutaka kesi hiyo kutupiliwa mbali kukataliwa na jaji anayesikiliza kesi hiyo kwa misingi kuwa muda wa kufanya hivyo ulikuwa umekwisha.Bashir anakabiliwa pia na mashitaka yanayohusiana na "kumiliki fedha za kigeni, ufisadi, na kupokea zawadi kinyume cha sheria", pamoja na mashitaka ya uchochezi na kuhusika katika mauaji ya waandamanaji.

Aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 na aliiongoza taifa hilo lililokuwa kubwa zaidi barani Afrika zama hizo hadi mwaka 2011 alipochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.

Alipochukua madaraka, Sudan ilikuwa katika mwaka wa 21 wa mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Kaskazini na Kusini

Japo serikali yake ilitia saini makubaliano ya kumaliza vita mwaka 2005, vita vingine vilizuka tena - katika eneo la magharibi mwa Darfur.

Bw. Bashir alituhumiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC kwa kupanga uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu katika eneo hilo.

Licha ya ICC kutoa waranti ya kimataifa ya kukamatwa kwake, alishinda uchaguzi mara mbili mwaka 2010 na 2015, japo vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi uliyopelekea ushindi wake.

Japo alikubali kujitenga kwa Sudan Kusini, mtazamo wake kuhusu jimbo la Darfur - ambalo lilikumbwa na ghasia kuanzia mwaka 2003 haukubadilika.

Omar al Bashir alizaliwa mwaka 1944 katika familia ya wakulima kaskazini mwa Sudan, ambayo pia ni sehemu ya ukoo wa ufalme wa Misri.