Mali yaendelea kuwaachilia huru wanamgambo wa Kiislam
Imechapishwa:
Kundi la pili la wanajihadi, wameaachiwa huru nchini Mali, na ripoti zinasema ni njia moja ya kutaka mfanyakazi wa kujitolea, raia wa Ufaransa pamoja na mwanasiasa wa mali waliotekekwa na waasi kuaachiwa huru.
Wanajihadi 30 waliaachiwa huru Jumatatu na Jumanne ya wiki hii hali ambao inaaminiwa kuwa itachingia kuwachiliwa huru kwa Soumaila Cisse na raia wa ufaransa Sophie Petronin.
Hata hivyo Sébastien Chadaud-Pétronin, mwanae Sophie Pétronin, akihojiwa na RFI amesema ana matumaini ya kuachiliwa huru kwa mama yake.
Lakini kufikia sasa hakuna tangazo rasmi kuhusu kuachiliwa kwa Mfaransa huyo Sophie Pétronin, aliyetekwa nyara huko Gao karibu miaka 4 iliyopita.
Sébastien Chadaud-Pétronin aliwasili Bamako Jumanne alasiri, ili kuweza kuwapo katika tukio la kuachiliwa kwa mama yake.