MSUMBIJI-CORONA-AFYA

Msumbiji kuanzisha uchunguzi dhidi ya vyeti bandia vya COVID-19

Msumbiji ina visa vya maambukizi zaidi ya Elfu Tisa.
Msumbiji ina visa vya maambukizi zaidi ya Elfu Tisa. Yasuyoshi CHIBA / AFP

Wizara ya afya nchini Msumbiji, imesema itaanzisha uchunguzi wa kina jijini Mputo ilikubaini madai ya biashara ya utoaji wa vyeti bandia vya kudhibitisha maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Msumbiji inahitaji watu wanaosafiri kuingia katika nchi hizo kuonyesha vyeti ya kutokuwa na virusi vya Corona katika kipindi cha saa 72.

Nchi hiyo ina visa vya maambukizi zaidi ya Elfu Tisa.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.