COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Upinzani wataka Uchaguzi Mkuu kusogezwa mbele Cote d'Ivoire

Magazeti mengi nchini Cote d'Ivoire yanazungumzia kuhusu uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.
Magazeti mengi nchini Cote d'Ivoire yanazungumzia kuhusu uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba. ISSOUF SANOGO / AFP

Wanasiasa wa upinzani nchini Cote d'Ivoire sasa wanataka Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwisho wa mwezi huu kuahirishwa ili Tume ya Uchaguzi ifanyiwe mageuzi.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii imetolewa mbele ya wajumbe wa Jumuiya ya viongozi wa ECOWAS, Umoja wa Afrika na wale wa Umoja wa Mataifa waliofanya ziara nchini humo kutathmini hali ya kisiasa katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Uchaguzi unapoelekea kukaribia wanasiasa wa upinzani nao wameendelea kushinikiza kujiondoa katika kinyang'ayiro hicho rais Outtara anayewania kwa muhula wa tatu.

Hivi karibuni mgombea mwingine wa urais nchini Côte d’Ivoire ambaye pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu Pascal Affi N'Guessan, aliugana na mgombea mwingine wa upinzani Henri Konan Bedie, kuwataka wananchi wa taifa hilo kugoma na kuadamana ili kumshinikiza rais Alassane Ouattara kutowania urais kwa muhula wa tatu.