DRC-RWANDA-UGANDA-USALAMA-MAENDELEO

Viongozi wa DRC, Uganda na Rwanda kujadili hali ya usalama na maendeleo katika nchi zao

Rais wa DRC Félix Tshisekedi ziarani Goma, Kivu Kaskazini, Aprili 14, 209.
Rais wa DRC Félix Tshisekedi ziarani Goma, Kivu Kaskazini, Aprili 14, 209. ALEXIS HUGUET / AFP

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Thisekedi leo anaongoza kikao cha viongozi wa nchi jirani kujadili hali ya usalama na maendeleo katika eneo hilo baada ya kuahirishwa mara kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

Kikao hiki kitafanyika kwa njia ya video kutokana na janga la Corona na kuwaleta pamoja marais wengine wa Uganda na Rwanda.

Awali kikao hicho kilikuwa kiwakutanishe marais watano, lakini ripoti zinasema kuwa rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, na mwenzake wa Angola Joao Lourenço walikuwa hawajathibitisha kushiriki katika kikao hicho muhimu.

Kabla ya kikao cha Jumatano, watalaam wa masuala ya usalama na Mawaziri wa Mambo ya nje, walikutana kufanya maandalizi ya kikao hiki kujadili ajenda muhimiu ya usalama.

Viongozi hao wanatarajiwa kuja na mapendekezo yatakayosaidia kuimarisha hali ya usalama na kukabiliana na makundi ya waasi, hasa Mashariki mwa DRC, katika eneo ambalo limeshuhudia mashambulizi yanayotekelewza na makundi ya waasi na kuendelea kusababisha maafa makubwa ya raia.

Rais Thsisekedi ambaye yupo mjini Goma, na amekuwa akwataka viongozi wa eneo hilo kujadili suala la amani na usalama.