COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

AU na UN watiwa wasiwasi na hali ya kisiasa nchini Cote d'Ivoire

Une vue de la ville d'Abidjan, de la lagune Ébrié et du Plateau depuis la cathédrale St-Paul.
Une vue de la ville d'Abidjan, de la lagune Ébrié et du Plateau depuis la cathédrale St-Paul. © Craig Pershouse / Getty Images

Ujumbe kutoka Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, umeonesha wasiwasi wao kuhusu joto la kisiasa nchini Cote d'Ivoire kuelekea Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika mwisho wa mwezi huu.

Matangazo ya kibiashara

Pamoja na wajumbe kutoka nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, wawakilishi hao wamekuwa nchini Cote d'Ivoire na kufanya mazungumzo na serikali, wapinzani na viongozi wa mashirika ya kiraia kuhusu uchaguzi huo.

Ziara hii imekuja wakati huu wapinzani wanapoendelea kushinikiza kuahirishwa kwa Uchaguzi huo, na kumtaka rais Allasane Outtara anayewania wadhifa huo kwa muhula wa tatu kujiondoa.

Aidha, shinikizo nyingine ni kwa Tume ya Uchaguzi kufanyiwa mageuzi kabla ya uchaguzi huo unaokaribia kufanyika.

Maandamano yamekuwa yakishuhidwa nchini humo, lakini serikali ya rais Outtara inaendelea kusisitiza kuwa uchaguzi huo wa Oktoba 31 lazima ufanyike.

Ujumbe wa ECOWAS ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana Shirley Ayorkor Botchwey, unasema unahofia matamshi ya chuki na matamshi ya kikabila huenda yakasababisha machafuko iwapo yataendelea kushuhudiwa.

Wiki iliyopita, shirika la kimataifa la kutatua Migororo International Crisis Group, nalo lilipendekedza uchaguzi huo kuahirishwa.