BURKINA FASO-MAUAJI-USALAMA

Burkina Faso: Zaidi ya watu 25 wauawa katika shambulio dhidi ya msafara wa wakimbizi

Watu zaidi ya 20 hawajulikani waliko, kulingana na mamlaka nchini Burkina Faso, baada ya shambulio dhidi ya msafara wa wakimbizi wa ndani walio kuwa wanarejea katika vijiji vyao katika mkoa wa Kaskazini.

Barabara inayoelekra Pissila (picha ya kumbukumbu).
Barabara inayoelekra Pissila (picha ya kumbukumbu). Flickr.com CC BY-NC 2.0 Rita Willaert
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne wiki hii. Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbi UNHCR limebaini kwamba watu wasiopungua 25 waliouawa katika shambulio hilo.

Watu hao walikuwa wamekimbia mashambulizi ya makundi yenye silaha. Baada ya kuona kuwa hali ya utulivu imerejea, waliamua kurudi katika vijiji. Msafara huo ulikuwa unajumuishwa na karibu wakimbizi 50 wa ndani.

Wauaji haoa ambao walikuwa kwenye pikipiki na gari ndogo walipora chakula chao.

Msafara huo uliviziwa kwenye umbali wa kilomita kumi kutoka mji wa Pissila. Wanawake na watoto walitenganishwa na wanaume. Wanaume tu ndio waliolengwa katika shambulio hilo. Kulingana na shahidi aliyejeruhiwa kwa risasi, wanaume waliotekwa walitenganishwa kwa makundi mawili. Karibu saa tano usiku ndipo wanaume hao walifyatuliwa risasi.

Kulingana na chanzo kutoka eneo la tukio, watu zaidi ya ishirini au waliotekwa nyara bado hawajapatikana. "Hakuna manusura au miili iliyopatikana bkufikia sasa," kilisema chanzo hiki. Vikosi vya ulinzi na usalama bado vinaendelea kutafuta watu ambao wako hai au miili ya ya watu watakao kuwa wameuawa.

Watu walionusurika kuuawa wamewasili Pissila. Katika taarifa yake, shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi limelaani vikali shambulio hilo dhidi raia.