DRC-RWANDA-ANGOLA-UGANDA-USALAMA

Suala la ukosefu wa usalama latawala mkutano mdogo wa kikanda Goma

Mwenyeji wa mkutano wa marais wanne, Félix Tshisekedi ameshiriki kutoka Goma.
Mwenyeji wa mkutano wa marais wanne, Félix Tshisekedi ameshiriki kutoka Goma. ISSOUF SANOGO / AFP

Baada ya kuahirishwa mara kadhaa, mkutano wa kilele kati ya wakuu wa nchi za DRC, Rwanda, Uganda na Angola umefanyika kwa njia ya video Jumatano (Oktoba 7).

Matangazo ya kibiashara

Mwenyeji wa mkutano huo, rais wa DRC, Félix Tshisekedi, ameshiriki mkutano huo kutoka mji wa Goma, mpakani na Rwanda. Mada kadhaa ziligubika ajenda ya mkutano, lakini maswala ya usalama yalichukua muda mrefu.

Marais kutoka mataifa manne kutoka ukanda wa Maziwa Makuu, wamekubaliana kuunganisha nguvu katika vita dhidi ya makundi ya waasi, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, pamoja na masuala mengine ya maendeleo kati ya nchi hizo.

Marais hao wamelaani mashambulizi yanayoendelea kufanywa na makundi ya wapiganaji hao,huku wakitilia mkazo umuhimu wa kuzuwia ufadhili wao na biashara haramu ya raslimali kwenye ukanda huo.

Hili limefikiwa baada ya kikao kufanyika siku ya Jumatano kwa njia ya video kikiongozwa na rais wa DRC Felix Thisekedi, pamoja na wenzake kutoka Uganda, Rwanda na Angola.

Mkutano huu umefanyika baada ya kuahirishwa mara mbili baada ya nchi hizo kutofautiana kuhusu ajenda.

Hata hivyo Burundi haikushiriki mkutano huo licha ya kualikwa rasmi.