GUINEA-UN-SIASA-USALAMA

UN yaonya kuhusu matamshi ya kisiasa yenye lengo la kuchochea machafuko Guinea

Siasa nchini Guinea zinaegemea sana ukabila na kunatarajiwa ushindani mkali kutoka kwa rais Alpha Conde, anayesaka muhula wa tatu na kuungwa mkono na kabila la Malinke, huku mpinzani wake Cellou Dalein akiungwa mkono na kabila la Fulani.
Siasa nchini Guinea zinaegemea sana ukabila na kunatarajiwa ushindani mkali kutoka kwa rais Alpha Conde, anayesaka muhula wa tatu na kuungwa mkono na kabila la Malinke, huku mpinzani wake Cellou Dalein akiungwa mkono na kabila la Fulani. REUTERS/Afolabi Sotunde/File Photo

Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu matamshi ya kikabila yanayoshuhudia nchini Guinea kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 18. Alpha Condé atawania katika uchaguzi wa urais kama ulivyotaka Mkutano Mkuu wa chama chake uliokutana Agosti 5 na 6.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Tume ya Umoja huo kuhusu Haki za Binadamu Michelle Bachelet anaonya kuwa, matamshi hayo yanatishia machafuko na ubaguzi na kuwataka wanasiasa kuacha kutoa matamshi yanayotishia usalama wa wananchi.

Siasa nchini Guinea zinaegemea sana ukabila na kunatarajiwa ushindani mkali kutoka kwa rais Alpha Conde, anayesaka muhula wa tatu na kuungwa mkono na kabila la Malinke, huku mpinzani wake Cellou Dalein akiungwa mkono na kabila la Fulani.

Hivi karibuni rais wa Guinea Alpha Conde, mwenye umri wa miaka 82, alitangaza kuwa anawania muhula wa tatu katika uchaguzi wa hapo Oktoba 18, akithibitisha mipango ambayo ilitarajiwa kwa muda mrefu.

Maandamano dhidi ya mpango wake ulioshukiwa wa kugombea tena yalizuka katika taifa hilo la Afrika magharibi Oktoba mwaka jana lakini yalikumbana na ukandamizaji wa nguvu, na watu kadhaa walipoteza maisha.

Conde, akiwa mwishoni mwa muhula wake wa pili na wa mwisho madarakani, alisukuma  mabadiliko ya katiba mwaka huu ambayo wapinzani wanasema yalipangwa kubadilisha muda wa kugombea.