GUNIEA-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Kiongozi wa upinzani Guinea Dalein Diallo amtaka rais Conde kustaafu

Cellou Dalein Diallo katika mahojiano na RFI na France 24, Oktoba 8.
Cellou Dalein Diallo katika mahojiano na RFI na France 24, Oktoba 8. RFI

Mgombea wa upinzani nchini Guinea amemtaka rais wa nchi hiyo Alpha Conde mwenye umri wa miaka 82 "kustaafu kwa heshima" kabla ya uchaguzi wa mwezi huu.

Matangazo ya kibiashara

Cellou Dalein Diallo, ndiye mshindani mkuu wa Alpha Conde katika uchaguzi wa Oktoba 18, ambapo rais anatafuta muhula wa tatu wenye utata.

Akizungumza katika mahojiano maalum na vituo vya France 24 na RFI, kiongozi huyo amesema kwa 'umri alionao Alpha Conde hana uwezo wa kuhudumu, kimuili na kiakili kutekeleza jukumu lake'.

Upinzani nchini Guinea umegawanyika kuhusu swala la uchaguzi, ambapo baadhi ya vyama vimetoa wito kwa wafuasi wao kususia uchaguzi huo kwa kile wanachokiita muhula haramu wa rais Alpha Conde.