COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Uchaguzi wa urais Cote d'Ivoire: Upinzani waandaa maandamano makubwa Abidjan

Muungano wa upinzani unataka Alassane Ouattara kutowania muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais ujao.
Muungano wa upinzani unataka Alassane Ouattara kutowania muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais ujao. SIA KAMBOU / AFP

Upinzani nchini Cote d'Ivoire unatarajia kufanya maandamano makubwa leo Jumamosi Oktoba 10. Maandamano hayo yanatia wasiwasi kwani vurugu za hapa na pale zimeendelea kuikumba nchi hii tangu mwezi Agosti kati ya wafuasi wa rais anaye maliza muda wake na wale wa upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka na vyama vya siasa wanahakikisha kuwa hatua zote za usalama zimezingatiwa.

Kulingana na upinzani nchini Cote d'Ivoire, makumi ya maelfu ya watu wanaweza kushiriki maandamano hayo kwenye uwanja wa Félix Houphouet Boigny.

Siku chache zilizopita, mkutano ulifanyika katika makao makuu ya chama cha PDCI kutoa mwongozo mpana wa 'mkutano wa huu mkubwa' huu.

Lengo kuu la mkutano huu wa maandalizi ni kuwahakikishia wanaharakati wa upinzani: "Tunawaalika wanaharakati wetu wote na raia wote wa Cote d'Ivoire ambao wanapenda amani na haki wajitokeze kwa wingi kusema hapana kwa ukiukaji wa sheria ya msingi ya nchi hii. Tunataka kuongeza kuwa hatua zote za usalama zimezingatiwa. Na kwa hivyo wananchi wa Cote d'Ivoire wanatakiwa kuondoa hofu kwenye akili zao.

"Onyo kutoka kwa mamlaka

Kwa upande wa mamlaka, wanasema hawana wasiwasi na mkutano huu. Mamadou Touré, msemaji wa serikali, ameonya watu wanaojaribiwa kwa kile alichokiita 'na maandamano ya vurugu'.

"Kuhusu maandamano haya ya upinzani, wako huru kuofanya maandamano kwa kuheshimu sheria na taratibu. Kile ambacho hatuwezi kukubali ni ujumbe wa chuki, hali inayoweza kuvuruga amani kuzoroteza shughuli za wengine. Lakini haya yote yakiheshimishwa, hakuna shida. "

Maafisa wengi wa polisi na askari wanatarajiwa kupelekwa katika maeneo mbalimbali ya mji wa Abidjan. Vyama vya upinzani vimetoa wito wa kuandamana kwa amani na pia vimeahidi kuwa vitashirikiana na vikosi vya usalama na ulinzi kwa kuzuia machafuko.