NIGERIA-USALAMA

Nigeria yavunja kikosi maalum cha polisi

Baada ya wiki moja ya maandamano nchini Nigeria, ofisi ya rais imedhinisha kuvunjwa kwa kikosi maalum (SARS), kinachotuhumiwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Mmoja wa waandamanaji wanaopinga ukatili wa polisi huko Ikeja akiandamana mbele ya maafisa wa polisi. Oktoba 9, 2020.
Mmoja wa waandamanaji wanaopinga ukatili wa polisi huko Ikeja akiandamana mbele ya maafisa wa polisi. Oktoba 9, 2020. PIUS UTOMI EKPEI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya hatua hiyo vijana wa Nigeria waliendelea na maandamano yao mwishoni mwa wikii iliyopita kuipnga kikosi hicho. Kabla ya maandamno hayo, wito mbalimbali ulitolewa kwenye mitandao ya kijamiina wanaharakati mbalimbali hususan vijana.

Kuanzia mwanzo, maandamano hayo yaliungwa mkono na nyota za mitinfo ya Afropop, ambao walipaza sauti na kutana jumuiya ya kimataifa kuingilia kati. Wanamuziki kama vile Davido au Wizkid wamekuwa wakituma taarifa mbalimbali kuhusiana na kikosi hicho cha polisi, wakiomba kivunjwe mara moja.

Wizkid alijiunga na kundi la raia wa Nigeria katika maandamano yaliyofanyika Jumapili hii, Oktoba 11 ijini London, nchini Uingereza.

Baada ya wiki moja ya maandamano, mkuu wa Polisi alitangaza kuvunjwa kwa kikosi cha kupambana na ujambazi, kulingana na matakwa ya waandamanaji. Wakati huo huo mkuu wa polisi aliahidi kuundwa kwa tume ya uchunguzi ili kuchunguza "uhalifu uliofanywa na polisi dhidi ya raia," ambao ambapo mashirika ya kiraia yatashirikishwa.

Nigeria imevunjilia mbali kikosi chake maalum cha polisi baada ya maandamano ya umma kutokana na madai ya ukatili wa polisi.