DRC-ELIMU

Mvutano waibuka kati ya walimu na serikali kuhusu kuanza kwa mwaka wa masomo DRC

(Shule ya Wangata) Nchini DRC, mwaka wa masomo umepangwa kuanza Oktoba 12, lakini vyama vya walimu vimeomba mwaka huo uahirishwe hadi Oktoba 26, 2020.
(Shule ya Wangata) Nchini DRC, mwaka wa masomo umepangwa kuanza Oktoba 12, lakini vyama vya walimu vimeomba mwaka huo uahirishwe hadi Oktoba 26, 2020. REUTERS/Kenny Katombe

Shule zote zimetakiwa kufunguliwa Jumatatu hii, Oktoba 12 nchi kote Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa mwaka wa masomo 2020-2021. Hatua iliyochukuliwa na serikali ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Walimu wanasema kwamba bado kuna matatizo mengi na mwaka wa masomo haungepaswa kuanza kwa sasa.

Wakati huo huo vyama vya walimu vimeamua kusogeza mbele mwaka wa masomo hadi Oktoba 26. Uamuzi huo umefutiliwa mbali na mamlaka ya Wizara ya Elimu.

Mwaka wa masomo uliopangwa kuanza Jumatatu hii nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeahirishwa DRC. Hali ambayo inaendelea kuzua sintofahamu kwa wazazi.

Kwa miaka kadhaa, maelfu ya walimu wamekuwa wanafanya kazi katika shule za umma bila hata kusajiliwa na serikali na wengi wao walikuwa hawalipwi mishahara yao. Ili kutarajia kupata ufadhili wa Benki ya Dunia ya dola milioni 200 mwishoni mwa mwaka huu, serikali inatarajia kuanza kuwalipa. Walimu 58,000 wanatarajia kupokea, kwa mara ya kwanza, mshahara wao mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba.

Ukaguzi wa walimu wa kweli na walimu hewa

Lakini kwa upande wa chama cha walimu wa DRC, sawa na chama cha walimu kutoka kanisa Katoliki katika ngazi ya taifa, wamesema hii sio habari njema. Wote wanaamini kuwa wale ambao wako kwenye orodha hiyo ni walimu hewa. Vyama hivyo viwili pia vilikutana na rais wa DRC, Felix Tshisekedi, mwezi wa Agosti ili kushtumu, na kuomba kushiriki katika ukaguzi huu mpya wa walimu. Lakini tangu wakati huo hakuna kilichofanyika.