MALI-UFARANSA-USALAMA

Mali: Ufaransa yadai kuwa na jukumu la pili katika mazungumzo kuhusu mateka

Mateka wa zamani wa Ufaransa Sophie Pétronin anashuka kwenye ndege kutoka Bamako baada ya kuachiliwa, katika uwanja wa ndege wa Villacoublay, Oktoba 9, 2020.
Mateka wa zamani wa Ufaransa Sophie Pétronin anashuka kwenye ndege kutoka Bamako baada ya kuachiliwa, katika uwanja wa ndege wa Villacoublay, Oktoba 9, 2020. GONZALO FUENTES / POOL / AFP

Siku nne baada ya kuachiliwa kwa Sophie Pétronin, Soumaila Cissé na mateka wawili wa Italia, bado kunaripoti hali ya sintofahamu. Ufaransa, kwa vyovyote vile, inahakikisha juu ya jukumu lake katika kuachiliwa kwa mateka hao.

Matangazo ya kibiashara

"Operesheni hiyo iliongozwa na Mali, masharti ya mazungumzo hayakuongozwa na Ufaransa." Huu ni ujumbe uliotolewa na ikulu ya Elysée, wakati mazingira ya kuachiliwa kwa Sophie Pétronin yameibua maswali mengi.

Ikiwa idara za usalama za mambo ya nje za nchi hizi mbili zilifanya kazi pamoja, Bamako ndio ilihusika sana katika suala hili, vyanzo vilivyo karibu na ofisi ya rais wa Ufaransa vimebaini. Vyanzo hivi vinahakikisha kuwa Paris haijalipa fidia.

Hata hivyo kuachiliwa huru kwa mateka wa Ufaransa, Sophie Pétronin, kumetoa angalizo kwa mateka wengine kutoka nchi za magharibi ambao bado wanashikiliwa, lakini pamoja nao, pia kuna idadi isiyojulikana ya mateka raia wa Mali na ukanda wa Sahel.

Juma lililopita watu zaidi ya 20 walitekwa katika tarafa ya Farabougou katikati mwa nchi ya Mali. 9 kati yao walikuwa bado wanashikiliwa mpaka Jumapili. Utekaji nyara unaolenga raia wa Mali wasiojulikana hautangazwi kama ule unaowahusu raia wa mataifa ya magharibi au wenyeji wanaofahamika kama vile kiongozi wa upinzani wa Mali Soumaila Cisse licha ya kuwepo wengine.

Ni vigumu kufahamu idadi yao kamili, lakini mtafiti kutoka taasisi ya ISS Ibrahim Maiga kutoka jijini Bamako amesema licha ya sababu tofauti za utekaji, lakini muhilmu ni kufahamu kwamba kuna wageni au wenyeji ambao ni wawakilishi wa serikali, wafanyabiashara, wanaoshikiliwa, inaweza kuwa zaidi ya 10 ambapo mara kadhaa wenyeji hupelekwa eneo ambalo sio mbali na sehemu walipotekwa.