COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Côte d'Ivoire: CEI yasema "iko tayari" kwa uchaguzi wa urais

Upinzani wa Cote d'Ivoire unashutumu Tume Huru ya Uchaguzi na kubaini kwamba kuna udanganyifu mkubwa uliopangwa.
Upinzani wa Cote d'Ivoire unashutumu Tume Huru ya Uchaguzi na kubaini kwamba kuna udanganyifu mkubwa uliopangwa. REUTERS/Luc Gnago

Kuanzia Jumatano hii Oktoba 14 hadi Oktoba 20, wananchi wa Côte d'Ivoire waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wataweza kupewa kadi zao za kupiga kura kwa ajili ay uchaguzi wa Oktoba 31.

Matangazo ya kibiashara

Ikiwa zimesalia siku 17 kabla ya uchaguzi wa urais, Tume ya Uchaguzi nchini Côte d'Ivoire, CEI, inasema "iko tayari". Upinzani, ambao ulitoa wito kwa watu kususia uchaguzi huo, bado haujaweka wazi mikakati yao na wagombea wake wawili bado hawajasema iwapo iwapo watashiriki katika uchaguzi huo wa urais au la.

Wapiga kura milioni 7.5 waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wanaweza kuanzia Jumatano wiki hii kwenda kwenye vituo vya kupigia kura kuchukuwa kadi zao za kupigia kura kwa uchaguzi wa urais.

"Ni vizuri kubaini kwamba wapiga kura wote, ambao ni kusema wapiga kura 7,495,082 kwenye waliojiandikisha wanahusika na zoezi hili la kupewa kadi hizi za wapiga kura, amesema Ibrahime Kuibiert Coulibaly mwenyekiti wa CEI . Tume huru ya uchaguzi iko tayari kuandaa uchaguzi wa urais wa Oktoba 31, 2020, tukisema kwamba hatutaki kuzua utata, wala kumzuia mtu yeyote. Kuheshimu Katiba na kanuni za uchaguzi tu ndio lengo letu, " CEI imesema latika taarifa.

CEI inasema iko tayari, lakini hali ya wasiwasi inatanda kuhusu uchaguzi huu wa tarehe 31.