DRC-AJALI-USALAMA

DRC: Kumi na nne wafariki katika ajali ya barabarani Kasai

Maafisa wakuu wa serikali mjini Mbuji Mayi wamesema kuwa idadi ya watu waliokufa katika Ajali ya barabarani kati ya Kinshasa na Mbuji-Mayi, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imeongezeka na kufikia watu kumi na wanne.

Mwezi Agosti watu wengine 14 walipoteza maisha katika barabara hiyo, katika nchi ambayo mbali na changamoto za kiusalama, imeendelea pia kushuhudia miundo mbinu mibovu, hasa barabara.
Mwezi Agosti watu wengine 14 walipoteza maisha katika barabara hiyo, katika nchi ambayo mbali na changamoto za kiusalama, imeendelea pia kushuhudia miundo mbinu mibovu, hasa barabara. REUTERS/Giulia Paravicini
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema gari lililokuwa linasafirisha bidhaa na abiria kutoka Mbuji-Mayi kwenda jiji kuu Kinshasa, lilihusika katika ajali hiyo, baada ya dereva kukosa mwekeleo na kuanguka katika eneo la Matshia.

Miongoni mwa waliopoteza maisha ni wanawake watano waliofariki dunia katika eneo la ajali, huku wengine wakipoteza maisha wakipewa matibabu.

Hii sio mara ya kwanza kwa ajali kama hii kutokea katika barabara hiyo kati ya Mbuji-Mayi na Kinshasa.

Mwezi Agosti watu wengine 14 walipoteza maisha katika barabara hiyo, katika nchi ambayo mbali na changamoto za kiusalama, imeendelea pia kushuhudia miundo mbinu mibovu, hasa barabara.